niko hapa?

Tathmini hii itamruhusu mwalimu wa mtoto wako kujua ni kiasi gani Kiingereza mtoto wako anajua.

ELL ina imanisha nini?

ELL inaimanishs ujifunzaji wa lugha ya Kiingereza.

Itachukua muda gani kwa mtoto wangu kuwa na ujuzi wa Kiingereza?

Kwa wastani, inaweza kuchukua hadi miaka 7.

Lugha ya kijamii kawaida huendeleza lugha ya kwanza na kawaida kitaaluma huchukua muda mrefu kukuza.

Kuna tofauti gani kati ya lugha ya kijamii na ya kitaaluma?

Lugha ya kijamii ni lugha tunayotumia kila siku tunapozungumza na familia na marafiki.

Lugha ya masomo ni lugha tunayotumia kusoma na kuandika shuleni.

Kwa nini ni muhimu kuendelea kuzungumza lugha yangu ya nyumbani nyumbani?

Kuwa na ustadi mkubwa wa lugha ya nyumbani inaweza kusaidia watoto kujifunza lugha nyingine kama Kiingereza. Jambo la muhimu zaidi, kuchunga lugha yako ya nyumbani itasaidia mtoto wako kuungana na tamaduni yake na familia kubwa

Ninaweza kufanya nini kusaidia masomo ya mtoto wangu lugha ya Kiingereza nyumbani?

Unaweza kumsaidia mtoto wako kwa kuendelea kuzungumza lugha yako ya nyumbani. Kulingana na umri wa mtoto wako na kiwango cha Kiingereza, unaweza kutaka kusoma vitabu vya lugha mbili pamoja. Vitabu vya lugha za mwanzoni vinaweza kupatikana katika www.storybookscanada.ca. Maktaba ya Umma ya Burnaby pia ina vitabu vya lugha mbili pamoja na vitabu katika lugha nyingi.

Ustadi wa lugha ya mtoto wangu utapimwa lini tena?

Mtoto wako atakaguliwa kila wakati na mwalimu wao wa ELL shuleni. Kuna tathmini rasmi ambayo hufanyika kila mwisho wa mwaka wa shule, kawaida kati ya mwezi ya ine na ya sita. Tathmini hii itatokea katika shule ya mtoto yako wakati wa siku ya kawaida ya shule.

Ni aina gani za msaada ambazo mtoto wangu atapata shuleni?

Mtoto wako atapata msaada wa lugha ya Kiingereza kutoka kwa mwalimu wa ELL shuleni. Msaada huu unaweza kuwa katika darasa au kwa vikundi vidogo. Mwalimu wa ELL na mwalimu wa darasa pia wanaweza kufanya kazi pamoja kujadili njia za kumsaidia mtoto wako.